Marekani yataka vita Ukraine vikomeshwe ifikapo Juni

Rais wa Ukraine Volodymir Zelensky, amesema amepokea mualiko wa kuhudhuria mkutano ambao huenda ukawawahusisha wakuu wa nchi tatu za Urusi, Ukraini na Marekani ikiwa ni mara ya kwanza kama utafanyika mkutano huo, na kwamba Marekani imetaka vita vya Ukraine kukomeshwa ifikapo Juni.

Moja kwa moja

Na Yusuph Mazimu na Na Laillah Mohammed

  1. Marekani yataka vita Ukraine vikomeshwe ifikapo Juni

    a

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Rais wa Ukraine Volodymir Zelensky, amesema kwamba Marekani imeitaka nchi yake na nchi jirani ya Urusi kumaliza vita yao inayoendelea ifikiapo mwezi Juni mwaka huu.

    Kiongozi huyo ameongezea kwamba, pande hizo mbili zinazozozana zimepokea mualiko kuhudhudria kikao cha mazungumzo nchini Marekani wiki ijayo.

    ‘Marekani imependekeza kuwa kwa mara ya kwanza makundi yanayowakilisha mataifa hayo mawili - yafanye kikao cha ana kwa ana nchini Maekani wiki inayokuja, na kuongezea kwamba vikao hivyo vifanyike katiak mji wa Miami. Ukraine imethibitisha kushiriki kwenye mkutano huo,’ alisema.

    Washington na Moscow hawajalizungumzia suala hilo, ila Rais wa Marekani Donald Trump amekuwa akipendekeza wazo la kutaka vita hivyo kukoma na mzozo kumalizwa tangu aliporejea madarakani mwaka mmoja uliopita. Wakati huo huo, Urusi imeendeleza mashambulizi yake yanayolenga miundo mbinu mbalimbali ya nishati, hali inayosababisha maeneo mengi zaidi kukosa umeme.

    Katika taarifa aliyowasilisha mapema leo, Zelensky aliwaambia wanahabari kuhusu yaliyojiri katika vikao vilivyoandaliwa Abu Dhabi, ambavyo vilikamilika Ijumaa wiki hii, ambapo hakukuwa na ripoti yoyote kuhusu hatua iliyopigwa ya kutatua mzozo. Zelensky amesema; ‘Masuala magumu yamesalia yalivyo, magumu,’ ikiwemo suala la Urusi kukalia maeneo yaliyo chini ya himaya ya Ukraine, huku Ukraine ikitakiwa kuachilia maeneo hayo kumilikiwa kikamilifu an Urusi.

    Amesema kwamba, pande husika zilijadili, kwa mara ya kwanza, uwezekano wa kufanyika mkutano utakaowahusisha viongozi wa nchi hizo tatu, na wala sio wajumbe wa nchi hizo, ila ameonya kuwa ‘maandalizi maalumu‘ ni sharti yafanyike kwa hilo kufanikiwa.

    Alipoulizwa ikiwa kuna muda uliowekwa kwa makubaliano kuafikiwa, kiongozi huyo wa Ukraine alijibu: ‘Wamarekani wanasema wanataka kukamilisha kila kitu ifiakiapo mwezi Juni. Ni kwanini hilo lifanyike kabla ya msimu wa joto kali kuanza?’ aliendelea kusema. ‘Tunaelewa kuwa masuala yao ya ndani yatakuwa na uzito na athari kubwa kwenye mzozo huu kati yetu.’

  2. Umoja wa Mataifa walaani shambulizi dhidi ya magari ya misaada ya chakula Sudan

    s

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Umoja wa Mataifa umelaani vikali shambulizi lililotekelezwa na ndege isiyokuwa na rubani ambayo ililenga magari ya kubeba misaada ya chakula yaliyokuwa yakipeleka chakula cha msaada kwa familia zilizopoteza makazi yao kutokana na vita katika Jimbo la Kordofan lililopo Kaskazini mwa nchi hiyo siku ya Ijumaa.

    Kwa mujibu wa ripoti kutoka nchini humo, mtu moja aliuawa kwenye shambulio hilo huku wengine kadhaa wakijeruhiwa vibaya. Marekani pia imelaani shambulizi hilo na kusema kwamba kamwe haikubaliani na hatua ya kuwashambulia wahudumu wa misaada ya kibinadamu wenye kutoa misaada muhimu kwa waathirirwa katika vita.

    Malori hayo yaliyokodiwa na Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa - WFP yalikuwa yanaelekea msaada wa chakula karibu na mji mkuu wa jimbo hilo wa El Obeid yaliposhambuliwa.

    Katika hatua nyingine takriban watu 24 wakiwemo watoto 8 wameuawa katika shambulizi lingine linalodaiwa kutekelezwa na vikosi maalum vya wanamgambo vya RSF. Wapiganaji wa kundi hilo wanadaiwa kuvamia gari lililokuwa limebeba watu wasio na makazi waliokuwa wanatafuta hifadhi kwingineko.

    Shambulizi hilo lilitokea katika Jimbo la Kaskazini mwa nchi la Kordofan. Katika taarifa iliyotolewa Jumamosi, Muungano wa madakatari nchini humo (SDN) umesema kwamba gari hilo lilishambuliwa katika eneo la Dubeiker wakati ambapo raia walikuwa wanakimbia mapigano katika jimbo Jirani la Kordofan Kusini.

  3. Mvuvi aliwa na mamba akimkimbia tembo

    s

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Polisi nchini Zambia wamesema wkamba Mvuvi mwenye umri wa miaka 52 amefariki baada ya kushambuliwa na mamba alipokuwa akikimbia kutoshambuliwn a kundi la Tembo katika eneo la Mashariki mwa Zambia. Dean Nyirenda alikuwa na arejea nyumbani kutoka safarini alipokwenda kuvua samaki na wenzake siku ya Jumatano, alipokutana na kundi la Tembo njiani.

    Walifanikiwa kuwakimbia Tembo hao, huku Nyirenda akijipata matatani alipokimbilia mtoni akidhania anakwepa kushambuliwa na Tembo bahati mbaya akakutana na mamba katika mto wa Luwangwa. ‘Hapo ndipo alipomshambulia kwa kuumwa mguu wake wa kulia,’ Mkuu wa polisi katika Eneo hilo Robertson Mweemba aliwaambia wanahabari.

    Taifa hilo la Kusini mwa Afrika lina idadi kubwa ya tembo ambao mara kwa mara hushambulia watu, hali ambayo imesababisha vifo vya watu wengi kwa miaka mingi. Polisi wanasema kwamba Nyirenda alifanikiwa kujinasua kutoka kwenye mdomo wa mamba kwa kumgonga mnyama huyo kwa fimbo aliyokuwa ameibeba mkononi.

    ‘Alijivuta kutoka mtoni,’alisema Mweemba. Wavuvi wenzake wawili ambao walikuwa wanatazama kwa mbali, walikimbia kumsaidia na kumbeba kutoka kwa kingo za mto akiwa anatokwa na damu nyingi. ‘Walijaribu kudhibiti eneo ambapo damu ilikuwa inatoka kwa wingi, ila alifariki akiwa njiani kwenda hiospitalini,’ Polisi walisema.

    Maafisa wa huduma kwa wanyama pori walifika katika eneo la tukio na kupata kuwa alikuwa ameshambuliwa vibaya na mamba huyo. BBC imewasiliana na mamlaka nchini zambia kupata taarifa zaidi kuhusu kifo cha mvuvi huyo. Mto Luwanga ambao unapita katika mbuga ya wanyama ya Luwaga Kusini, ni makazi ya mamba aina ya Nile barani Afrika kwa mujibu wa takwimu za mashirika ya uhifadhi wa wanyama pori.

    Jumla ya vifo 26 vilivyotokana na wanyama pori na ambavyo viliripotiwa mwaka 2023, 15 vilitokana na watu kushambuliwa na mamba – wengi wao katika mto Luwanga – kwa mujibu wa shirika la kijami la Recource Africa.

    Mamlaka za kusimamia wanyama Pori zimesema kwamba zimekuwa zikiangazia kwa kina jinsi ya kupunguza na kudhibiti mashambulizi ya wanyama pori dhidi ya binadamu kwa kujenga uzio wa umeme karibu na maeneo ambayo ni makazi ya wanamya hao pori.

  4. Kenya yachunguza Watanzania wawili kwa tuhuma za kufadhili ugaidi

    C

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mamlaka nchini Kenya zimesema kwamba Watanzania wawili ni miongoni mwa watu 13 ambao wanaotuhumiwa kwa makosa ya kufadhili ugaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na wanakabiliwa na mashtaka na vile vile vikwazo vya kiuchumi.

    Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa kwa vyombo vya habari nchini Kenya, Mamlaka zimesema kwamba watuhumiwa 13, wakiwemo Wakenya 10 na Mganda 1 na watanzania hao wawili wanachgunguzwa kwa kuhusika na shughuli za kigaidi ikiwemo ufadhili wake, na majina yao yameshawasilishwa kwa taasisi kama vile Benki na nyinginezo za kiusalama kuchunguza kwa kina vyanzo vya fedha walizonazo na jinsi fedha hizo zinavyotumika.

    Hatua hiyo itazilazimu Benki husika kusimamisha akaunti za wahusika hao na kutoa taarifa muhimu kuhusu akaunti hizo kwa vyombo vya usalama nchini Kenya. Mashirika ya kutoa mikopo au huduma nyinginezo za kifedha zimeamrishwa kutofanya biashara na watu hao wakati huu ambapo uchunguzi kuwahusu inapoendelea.

    Kamati maalum ya baraza la mawaziri inayochunguza ugaidi na ufadhili wake nchini Kenya imesema kwamba watu hao wanatakiwa kufungiwa akaunti zao za benki. Serikali ya Kenya kupitia kituo cha kuripoti uhalifu wa kifedha {Financial reporting centre} imeorodhesha majina ya 13 hao.

    Watu aho ni Salehe Burhani Minja na Jerumani Koja kutoka Tanzania. Kutoka Kenya ni Violet Kemunto Omwoyo, Juma Ambare, Zakariya Kamal, Sufi Abasheikah, Jamal Abdi Mohammed na Hadija Issack Ali. Wengine ni Abdiweli Dubat Dege, Ramadhani Hamisi Kufungwa, Robert Karani Nyokae, Suena Nakhumicha Machabe, na Mohammed Siyat Ali huku mganda pekee ni Abubakar Swaleh.

  5. Trump atishia kuongeza ushuru kwa mataifa yanayofanya biashara na Iran.

    s

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Rais wa Marekani Donald Trump ametia saini amri nyingine ya Rais inayotishia kuyawekea ushuru zaidi mataifa yanayoendelea kufanya biashara na Iran. Amri hiyo iliyotolewa Ijumaa, haitoi maelezo zaidi kuhusu viwango vya ushuru utakaotozwa, ila umetoa mfano wa ushuru wa asilimia 25.

    Imesema pia kwamba ushuru huo utatozwa dhidi ya bidhaa ambazo zinatoka Marekani kuelekea nchi nyingine ‘kupita mfumo wa kuagiza moja kwa moja au kwa kupitia njia nyingine’. Aidha imeendelea kusema kwamba kununua bidhaa, kuingiza bidhaa au kupata bidhaa kutoka Iran, itakuwa ni sababu ya kutozwa ushuru zaidi na Marekani.

    Trump hajazungumzia suala hilo moja kwa moja, ila ameisitiza kwamba ‘Iran haitokubaliwa kamwe kumiliki silaha za kinyuklia’ alisema akiwa safarini kwenye ndege ya rasmi ya Rais wa Marekani – AIRFOCE ONE. Haya yanajiri wakati ambapo mazungumzo yanaendelea kati ya Marekani na Iran kule Oman, kufuatia wiki kadhaa ya vitisho kutolewa kutoka pande zote mbili.

    Trump alitishia kuongeza ushuru wa asilimia 25 kwa mataifa yanayofanya biashara na Iran mapema mwaka huu, katika tangazo alilochapisha kwenye mtandao wake wa kijamii wa TRUTH SOCIAL. Januari 12, aliandika: ‘Kuanzia sasa, taifa lolote ambalo litafanya biashara na Iran litatozwa ushuru wa asilimia 25 kwa biashara zote ambazo zinashirikisha Marekani. Wakati huo, hakukutolewa taarifa zaidi jinsi ushuru huo ungetozwa au kutekelezwa.

  6. Mmiliki wa Mochwari afungwa miaka 40 kwa kudhalilisha maiti

    S

    Chanzo cha picha, CBS

    Jon Hallford, mmiliki mwenza wa nyumba ya kuhifadhi maiti 'Mochwari' na kuzika inayoitwa “Return to Nature” huko Penrose, Colorado, amehukumiwa kifungo cha miaka 40 jela baada ya kubainika kuwa karibu maiti 200 zilihifadhiwa vibaya.

    Hallford alitahadharisha Mahakamani na kusikia familia zikielezea hofu walizopata kuona wapendwa wao wakidhalilika chini ya huduma yake. Baadhi ya familia walimtaja Hallford kama “mtu katili” anayestahili kuangamia gerezani.

    Mke wake wa zamani na mmiliki mwenza, Carie Hallford, amekiri makosa hayo pia na anasubiri hukumu.

    Mochwari hiyo ilikuwa ikiwapa familia majivu bandia badala ya mabaki halisi ya wapendwa wao. Mahakama ilibaini kuwa maiti 189 zilihifadhiwa vibaya kwa zaidi ya miaka minne. Familia za ndugu wa marehemu zilizokusanyika mahakamani ziliomba apewe kifungo cha juu zaidi cha miaka 50.

    Hallford alikiri makosa yake na kusema:

    “Nilikuwa na fursa nyingi kuacha yote, lakini sikufanya. Makosa yangu yataendelea kuathiri vizazi vijavyo.”

    Mawakili wa serikali walisema familia hiyo ilikuwa ina tamaa, huku ikiwa na uwezo wa kutunza maiti vizuri. Mochwari hiyo ilikuwa ikihifadhi maiti na kufanya mazishi bila kemikali, ikitumia jeneza linaloharibika haraka.

    Vilevile, uchunguzi ulianza baada ya malalamiko ya harufu mbaya kutoka kwenye nyumba hiyo. Maiti zilizobainika zikiwa jumla ya 115 zilikusanywa mwanzoni mwa Oktoba mwaka uliopita.

  7. Museveni kuwasili leo Tanzania kwa ziara ya kikazi ya siku 1

    s

    Chanzo cha picha, Ikulu Uganga/PPU

    Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, anatarajiwa kuwasili nchini Tanzania leo Jumamosi, Februari 7, 2026, kwa ziara ya kikazi ya siku moja.

    Museveni atakutana na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambapo mazungumzo yao yatajikita katika kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizi mbili, na kujadili masuala muhimu ya kikanda na kimataifa.

    Miongoni mwa masuala makuu yatakayojadiliwa ni mradi wa bomba la mafuta ghafi Afrika Mashariki (EACOP), unaotarajiwa kuleta faida kwa nchi zote mbili na kanda kwa ujumla.

    Ziara hii ni ya kiongozi wa kwanza wa kimataifa kufika Tanzania baada ya uchaguzi mkuu wa Tanzania wa Oktoba 29, 2025 ulioshuhudia ghasia zilizosababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali, na pia ni ziara ya kwanza ya Museveni nje ya nchi tangu kuanza muhula wa 7 Januari 15, 2026, akiongoza Uganda tangu mwaka 1986.

  8. Polisi wa Kenya waliokuwa Haiti waanza kurejea nyumbani,

    s

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Leo Jumamosi Februari 7 2026 ndio siku ya mwisho ya kikosi cha misheni ya kimataifa inayosimamia usalama nchini Haiti (MSS) kuhudumu nchini humo. Kufuatia hatua ya wafadhili wakuu kama vile Marekani na Umoja wa mataifa kuamua kusitisha misheni hiyo na kubuni operesheni mpya, vikosi vya usalama vilivyokuwa vikiongozwa na polisi wa Kenya vimekuwa vikijiondoa nchini humo tangu mwezi Desemba mwaka jana.

    Kwa mujibu wa Katibu Mkuu katika wizara ya Mambo ya Kigeni, Sing’oei Korir ; ‘ Kenya tayari imepiga hatua kubwa kabisa katika sekta ya kutoa usalama wa kimataifa hasa katika maeneo ambayo yanakumbwa na changamoto za kiusalama kama vile Haiti.’

    Kundi la kwanza la polisi 400 lilirejea nchini mwishoni mwa mwaka jana, huku Marekani ikituma vikosi vyake katika taifa hilo la Caribbea. Kenya ambayo ilikuwa ikiongoza misheni hiyo ya kukabiliana na magenge yanayodhibiti hususani Mji Mkuu Port Au Prince ilikuwa na kikosi kikubwa cha maafisa 735.

    Guetamala iliwatuma polisi 150, El Salvador 78, Jamaica 3, Bahamas 1 na 7 kutoka Canada. Japo Kenya imejivunia kuwa na mafanikio makubwa katika juhudi zake kupambana na utovu wa usalama katika taifa hilo, iliwapoteza maafisa wawili waliouawa katika uvamizi uliotekelezwa kwenye gari lao walipokuwa wakishika doria mjini.

    Misheni ya MSS ilianza operesheni zake nchini Haiti mnamo Juni 2024 baada ya Rais William Ruto kupata idhini ya bunge la Kenya kuwatuma maafisa wa polisi kuhudumu katika misheni hiyo. Hata hivyo ilicheleweshwa awali kutokana na baadhi ya raia kuwasilisha kesi mahakamani kupinga mkataba uliotiwa saini kati ya Kenya na aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo wakati huo Ariel Henry.

    Kinara wa chama cha ThirdWay Alliance, Wakili Ekuru Aukot aliwasilisha kesi mahakamani akipinga mkataba huo kwa kudai kwamba Haiti wakati huo haikuw ana serikali kamili inayoweza kutoa ombi la kutaka msaada kutoka kwa taifa kama Kenya.

    Mahakama ilisimamisha polisi kutosafiri hadi Haiti kwa muda kabla ya Rais kuwasilisha hoja hiyo katika bunge la Taifa ambapo alipata uungwaji mkono kutokana na chama chake cha UDA kuwa na idadi kubwa ya wabunge katika bunge hilo. Wakati huu ambapo misheni hiyo inakamilika Kenya inajipa moyo kwa kuweza kutekeleza operesheni yake ya kwanza inayoongozwa na kikosi cha polisi.

    Katika miaka ya nyuma, Kenya imevituma vikosi vyake katika misheni za kudumisha amani katika mataifa kama vile Namibia, Yugoslavia, Bosnia, Liberia , Sierra Leone, huku KDF ikihudumu kwa pamoja na maafisa wa polisi kutoka Kenya katika misheni ya kudumisha amani nchini Somalia AUSSOM.

    ‘Tumefanya kazi iliyotupeleka huko, ambayo ni kudumisha amani na utulivu wa kiwango kinachowezekana,’ alisema Katibu Mkuu Korir na kuongeza; ‘Tuko pahali pazuri pa kuwaondoa maafisa wetu wakati huu.’

    Mwaka 2025 Umoja wa mataifa uliidhinisha uwepo kwa misheni mpya nchini Haiti inayofahamika kama GANG SUPPRESSION FORCE ambayo itakuwa na maafisa 5500 kutoka mataifa mbali mbali duniani. Misheni hiyo itajumuisha vikosi vya mataifa kama vile Marekani, Canada, Kenya, The Bahamas, Jamaica, Guatemala na El Salvador.

    Na tofauti na ile ya MSS, jukumu kuu la misheni hii mpya litakuwa kutumia mbinu tofauti za kukabiliana na tatizo lililopo kwa kudumisha usalama, kutumia ujasusi kudhibiti mashambulizi zaidi na kuvunja makundi ya magenge yaliyodhibiti baadhi ya maeno ya mji mkuu Port Au Prince, kuzuia kuingia na usambazaji wa silaha ndogo na kuweka mazingira ambayo yatawezesha siasa za kiraia kuimarika nchini humo.Kwa baadhi ya raia, kuondoka kwa kikosi cha Kenya kina leta matumaini na pia hofu ya hali itakavyokuwa kabla ya kikosi kipya kuanza kazi huko.

  9. Trump afuta video ya ubaguzi wa rangi dhidi ya Obama, asema hataomba msamaha

    s

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Rais wa Marekani, Donald Trump, amefuta video yenye kipande cha ubaguzi wa rangi alichochapisha kwenye mitandao ya kijamii kilichomlinganisha Rais wa zamani Barack Obama na Mkewe Michelle Obama na sokwe. Hata hivyo, kwa mujibu wa NBC News Trump amesema hataomba msamaha kwa kuchapisha video hiyo.

    Video hiyo, yenye muda wa takribani dakika moja, ilihusu madai ya udanganyifu kwenye uchaguzi wa mwaka 2020, lakini mwishoni ilionyesha sura za familia hiyo ya Obama zilizopachikwa juu ya vichwa vya sokwe huku wimbo wa “The Lion Sleeps Tonight” ukipigwa.

    Akizungumza na waandishi wa habari Ijumaa usiku, Trump alisema:

    “Bila shaka nakataa sehemu za ubaguzi wa rangi za video hii, lakini sina mpango wa kuomba msamaha.”

    Awali, Ikulu ya Marekani ilijitetea kwa kusema video hiyo ilitoka kwenye video ya vichekesho vya mtandaoni 'meme' vya mtandaoni, lakini baada ya kupokelewa kwa hasira kutoka kwa waaharakati na baadhi ya wanasiasa wakiwemo wa chama chake, video hiyo ilifutwa.

    Msemaji wa Ikulu alisema:

    “Mfanyakazi mmoja wa Ikulu kwa bahati mbaya alichapisha video hiyo. Tayari imefutwa.”

    Trump hakujibu moja kwa moja Ijumaa usiku kuhusu ni mfanyakazi gani alichapisha video hiyo au kama atafutwa kazi.

  10. Marekani yasifu mazungumzo na Iran, Trump asema yameanza vyema

    s

    Chanzo cha picha, AFP/East News/Radio Zet

    Rais wa Marekani Donald Trump amesema mazungumzo ya kiwango cha juu kati ya Marekani na Iran yaliyofanyika Oman yamekamilika vyema na kwamba pande zote mbili zitaleta kikao kingine wiki ijayo, ingawa hakutoa maelezo zaidi kuhusu mkutano huo.

    “Tulikuwa na kikao kizuri sana na mwakilishi wa juu kutoka Iran, na tutaona matokeo yatakavyokuwa,” Trump alisema mbele ya waandishi wa habari akiwa ndani ya ndege ya Air Force One na kunukuliwa na NBC News. Aliongeza kuwa Iran haiwezi kuruhusiwa kuwa na silaha za nyuklia chini ya makubaliano yoyote.

    “Tutakutana tena mwanzoni mwa wiki ijayo, na Iran wanataka kufanya makubaliano, kama inavyopaswa. Wanajua matokeo kama wasipofanya makubaliano. Yatakuwa makubwa sana. Tutaona yanayofuatia,” Trump alisema.

    Kwa mujibu wa maafisa wa Marekani, mazungumzo hayo hayakuwa ya ana kwa ana, bali pande zote ziliwasilisha msimamo wao kwa usimamizi wa Oman.

    Mvutano kati ya Marekani na Iran umekuwa ukiongezeka, huku Trump akirudia kuonya kuhusu uwezekano wa shambulio la kijeshi. Vilevile, Marekani ilionyesha wazi uwezekano wa kuingilia kati kijeshi.

    Kwa upande wa Iran, Waziri wa Mambo ya Nje Abbas Araghchi, alieleza kuwa mazungumzo hayo yalianza vyema. “Hii ilikuwa ni mwanzo mzuri. Hatua zinazofuata zitaamuliwa baada ya mashauriano ya ndani,” alisema kupitia ujumbe wa maandishi uliotumwa kwa vyombo vya habari ndani ya Iran.